Thursday, November 9, 2017

EL SHAARAWY AWEKA REKODI

Usiku wa October 31 2017 michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya maarufu kama UEFA Champions Leagueiliendelea kwa michezo nane kuchezwa barani Ulaya, Barcelona walikuwa ugenini kucheza dhidi ya Olympiakosgame ambayo imemalizika kwa sare tasa.
Chelsea walikuwa Italia kucheza dhidi ya wenyeji wao As Roma na kujikuta wanakubali kipigo cha magoli 3-0 wakati Manchester United walikuwa nyumbani Old Trafford kucheza dhidi Benfica ya Ureno game ambayo imemalizika kwa Man United kupata ushindi wa magoli 2-0.
Game ya Chelsea dhidi ya AS Roma ndio game ambayo ilikuwa inatajwa kuwa itavuta hisia za mashabiki wengi kutokana na Chelsea na Roma zote zipo katika kiwango kizuri na katika msimamo wa Kundi C zilikuwa zinafukuzana.Chelsea wamekubali kipigo cha magoli 3-0 dhidi ya AS Roma magoli ya Roma yakifungwa na Stephen El Shaarawy aliyefunga magoli mawili dakika ya 1 na dakika ya 34.
Msimamo wa Kundi C ulivyo kwa sasa
Magoli hayo yamemfanya Stephen El Shaarawy kuweka rekodi ya kufunga magoli mawili katika game moja ya UEFA Champions League kwa mara ya kwanza katika maisha yake ya soka na baadae Diego Perotti akafunga goli la tatu dakika ya 63.

DIAMOND VS ALI KIBA

Muda mfupi baada ya mwimbaji staa Alikiba kuachia video ya wimbo wake mpya ‘Seduce Me’ leo August 25, 2017, staa mwingine wa Bongofleva kutokea WCB, Diamond Platnumz amepost picha kwenye Instagram.
Diamond amepost picha ya mtu akicheka kitu kilichowafanya mashabiki kuunganisha matukio wakidai huwenda picha hiyo ni ujumbe baada ya kuusikia wimbo wa Alikiba.

MLIPUKO KAGERA


Mapema leo November 8, 2017 kulisambaa taarifa kutokea Kanda ya Ziwa hasa Mkoa wa Kagera zikieleza kuwa kitu kinachodhaniwa kuwa bomu, kimelipuka katika Shule ya Msingi Kihinga iliyopo kijiji cha Kihinga kilichopo Kata ya Lulenge wilayani Ngara na kusababisha majeruhi.
 imempata Mganga wa Hospitali ya Rulenge iliyopo wilayani Ngara, Kagera, Sister Mariagoreth Fransis ambaye amesema wamepokea majeruhi 45 waliotokana na mlipuko huo ambapo kati ya majeruhi hao, 13 wamejeruhiwa vibaya na wawili wamefariki.

EL SHAARAWY AWEKA REKODI

Usiku wa October 31 2017 michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya maarufu kama  UEFA Champions League iliendelea kwa michezo nane kuchezwa barani...