
Usiku wa October 31 2017 michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya maarufu kama
UEFA Champions Leagueiliendelea kwa michezo nane kuchezwa barani Ulaya,
Barcelona walikuwa ugenini kucheza dhidi ya
Olympiakosgame ambayo imemalizika kwa sare tasa.
Chelsea walikuwa Italia kucheza dhidi ya wenyeji wao As Roma na kujikuta wanakubali kipigo cha magoli 3-0 wakati Manchester United walikuwa nyumbani Old Trafford kucheza dhidi Benfica ya Ureno game ambayo imemalizika kwa Man United kupata ushindi wa magoli 2-0.

Game ya
Chelsea dhidi ya
AS Roma ndio game ambayo ilikuwa inatajwa kuwa itavuta hisia za mashabiki wengi kutokana na
Chelsea na
Roma zote zipo katika kiwango kizuri na katika msimamo wa
Kundi C zilikuwa zinafukuzana.
Chelsea wamekubali kipigo cha magoli 3-0 dhidi ya
AS Roma magoli ya
Roma yakifungwa na
Stephen El Shaarawy aliyefunga magoli mawili dakika ya 1 na dakika ya 34.

Msimamo wa Kundi C ulivyo kwa sasa
Magoli hayo yamemfanya Stephen El Shaarawy kuweka rekodi ya kufunga magoli mawili katika game moja ya UEFA Champions League kwa mara ya kwanza katika maisha yake ya soka na baadae Diego Perotti akafunga goli la tatu dakika ya 63.
No comments:
Post a Comment